KAMA KAZI YA CHUMBA NI KULALA TU BASI RAMANI HII INAKUFAA KWA WEWE MBANA MATUMIZI.

Habari wapendwa nashukuru kwa kuendelea kuipa nguvu blog hii,leo nawaletea ramani nzuri ndogo na inayoweza kujengwa na mtu wa kipato chochote,

Watu wengi hupenda kujenga majumba mkubwa kisha mwisho wa siku huwashinda kuyamaliza,
hata kama ikiisha basi ni kwakipindi kirefu sana, na ikiisha katika hiyo nyumba huishi baba mama na mfanyakazi mala chache labda na yule mtoto wa mwisho,

hii baada ya muda huleta usumbufu hasa wakati wa kuifanyia usafi hiyo nyumba,
wakati tunamalizia mwaka huu,nimekutana na mawazo tofauti ya wahitaji wa ramani mbalimbali,
mwingine anataka vyumba viwe vikubwa sana, mwingine anataka humohumo kwenye nyumba ya familia kuwe na gym,rest area,sebure mbili n.k.

leo nimekutana na huyu,
 yeye anataka ramani yake isiwe na vyumba vingi, anataka vyumba vitatu kimoja master,jiko,public toilet na master kubwa,

mawazo yake yanamwambia katika familia yake watoto ni wapangaji, akanipa mfano;
mtoto anapofikisha miaka mitano hadi saba anaanza darasa la kwanza na katika shule za siku hizi na uvivu wetu wa kulea watoto unawapeleka shule za kulala hukohuko, yeye akiludi nyumbani hasa wakati wa likizo tena atakaa kwakipindi cha mwezi mmoja tu,hapohapo atataka kwenda mikoani likizo kwa bibi au babu au shangazi,,,,

huyo ni mtoto wa shule ya msingi,ukija sekondali hali ni hivyohivyo boarding kila mahali, akienda chuo ndio kabisaa si wakuludi leo wala kesho,akimaliza chuo anapata kazi anajitegemea,hivyo huyu bwana watoto kwake ni wageni haoni sababu ya kawaandalia vyumba vikuubwa kwaajili yao,

sababu kubwa kabisa nyingine ya huyu bwana ni kubana matumizi, yeye anaamini nyumba ni aseti kubwa sana unapojenga nyumba moja ambayo thamani yake unaweza kujenga nyumba mbili hiyo ni asara kubwa kwake.

kama chumba cha watoto kazi yake nikulala tu basi kwake apate nafasi ya kuweka kitanda, labda na kakabati kadogo cha ukutani cha kuwekea nguo,,
lakini masterbedroom unaweza kuifanya kuwa kubwa uwezavyo,

sitaki kukuchosha na maneno ya huyu bwana anayesema  kama unataka kuishi na wazazi au mfanyakazi basi kujenga self ya chumba kimoja au viwili pembeni huwezi shindwa maana wazazi wanahitaji uhuru wa kuishi peke yao,
ramani anayoitaka itakua hivi,


SITTING AREA   4m X 4m
MASTER BEDROOM   3m  X 3.67m
2BEDROOMS   2m   X  2m (Bila kabati)
KITCHEN    2m X 1.5m   (Bila kabati)
PUBLIC TOILET   0.9m  X 2m


Kwa sifa hizo ramani hii itachukua
BLOCKS     1700
BRICKS    8500
CEMMENT KUJENGEA TOFARI 26 OR 47 BAGS
BATI ZA FUTI 10 ZIWE  55
MBAO ZA KENCHI 300


makadilio ya wastani unaweza kutumia milion47 hadi kuisha

Jumla yote ina upana 9.3m kwa urefu 7.9m hivyo inaingia hata kwenye kiwanja cha high density ya 15 X 15m.

nakuwekea na picha zake zote kama utaipenda tuwasiliane 0756230076 , 0783230076utaipata












KAMA KAZI YA CHUMBA NI KULALA TU BASI RAMANI HII INAKUFAA KWA WEWE MBANA MATUMIZI. KAMA KAZI YA CHUMBA NI KULALA TU BASI RAMANI HII INAKUFAA KWA WEWE MBANA MATUMIZI. Reviewed by Protas Sangu jr on Monday, December 26, 2016 Rating: 5

12 comments:

  1. Protasi Hii kitu nimeilewa sanaa ila utaniongezea tu sehemu ya kuswalia chumbani ktk Master au haina master?

    ReplyDelete
  2. samahani mkuu. je kwa nyumba za kijijini ile mtu anataka nyumba ya bati 40 za alaf za rangi alafu vyumba vitatu na sebule tuu haina hayo makorombwezo mengine nasaidikaje. anatarajia kutumia tofali za block

    ReplyDelete
  3. Samahan mkuu
    Kanyumba kadogo kavyumba viwili

    ReplyDelete
    Replies
    1. sawa tuwasiliane whatsap mkuu 0756230076

      Delete
  4. Nitumie ramani ya nyumba ya vyumba vitatu na sebule Ila chumba kimoja kiwe master bedroom

    ReplyDelete
  5. Samahani naomba kusaidiwa.je kwa million 4 inaweza jenga nyumba ya kulala yenye vyumba viwili ambayo choo ipo ndani kutumia kwa vyumba vyote viwili,sebule na jiko?

    ReplyDelete
  6. Nimeipenda ramani yako ya nyumba ya vyumba viwili tu. Nataka kujenga hivi karibuni kijijini na nahitaji ramani nzuri na ushauri wako, niweze timiza ndoto yangu. Jiko, sitting, dining na veranda ni muhimu kuzingatiwa. Asante sana.

    ReplyDelete
  7. Naomba ramani ya vyumbq 5 naseble

    ReplyDelete

Two bedroom kitchen and public toilet

 Bati 25 Tofali 2100 Ramani yake /complite drawings 0756230076, 0783230076


Powered by Blogger.